Fatuma

Uncategorized Comments (0)

Fatuma Kumekucha

Mama wa watoto watano, mke mnyenyekevu, na mkulima asiye na masihara.

Fatuma amejitoa kwa familia yake. Tangu asubuhi hadi machweo anafanya kazi za kuinufaisha familia yake kwa kutazama nyumba na kulima shamba la mumewe la heka tatu. Maisha yake ya ukulima ni magumu. Fedha ni haba. Kila wakati anawaza ataweza vipi kuilisha familia yake na pia kupata fedha kutokana na kilimo chake. Kila wakati inambidi kupima mustakabali wa lishe ya familia yake kabla ya kutumia fedha anayopata toka kwenye mauzo ya mazao yake. Ni lazima ahakikishe kuwa kuna chakula cha kuitosha familia nyumbani mwake.

» Uncategorized » Fatuma
On June 21, 2016
By

Comments are closed.

« »