Mashoto

Uncategorized Comments (0)

char-mashoto

Kijana mwenye Mori, mtafutaji, mpenzi, na mkulima chipukizi.

Mashoto ni kijana wa miaka 21, hana ajira ya kudumu na wala hategemei kuwa nayo. Shughuli zake ni za kuungaunga, kujipatia riziki ya siku. Amezaliwa na kukulia kijiji cha Lunyanja, siku zote amekuwa akiamini kuwa kilimo ni umasikini. Ameshuhudia mama yake akitaabika na kilimo hadi umauti wake.

Mashoto hana mipango ya kuwa mkulima. Ama kwa hakika Mashoto hana hakika anahitaji kufanya nini hasa na maisha yake. Anayo ndoto ya kwenda kupotelea mjini lakini maisha yasiyo na hakika yanambakiza hapa kijijini akijipatia fedha ya kula leo na kesho katika soko la Lunyanja.

Ni kitu gani kinachombakiza hapa Lunyanja? Cha kwanza ni msichana kinda na mrembo, Lightness. Dada huyu tayari amekwishakupata mtoto ambaye baba yake hajulikani aliko. Lightness ni mwenyeji wa hapa Lunyanja lakini anaonekana kuwa mtu mwenye maendeleo zaidi ya eneo aliko. Lightness na Mashoto wanakuwa wapenzi, mara baada ya Lightness kumzungusha kidogo bwana mdogo kutokana na tabia zake mbovu. Je Lightness atafanikiwa kumbakiza Mashoto Lunyanja, au jamaa kashakata shauri la kutokome mjini?

» Uncategorized » Mashoto
On June 20, 2016
By

Comments are closed.

« »