Lightness

Uncategorized Comments (0)

char-lightness

Mjukuu, mama, mkulima chipukizi.

Alipata mimba akiwa na miaka 16. Akafukuzwa toka nyumbani kwa wazazi wake huko Mbeya na akaamua kuja hapa Lunyanja kuja kuishi na bibi yake, Bibi Salama, ambaye anamiliki kilabu maarufu cha pombe hapa kijijini.

Lightness anamhudumia mwanawe, Davido, yeye peke yake kwa kusaidia kazi katika kilabu cha Bibi Salama, na pia katika kipande chao kidogo cha shamba. Amejifunza kukaa chonjo na umbea wa kijiji, na pia wanaume manyang’au wanaodhani Lightness anahitaji. Lightness ana ishi kwa kujiamini na ni msichana mwenye msimamo.

» Uncategorized » Lightness
On June 20, 2016
By

Comments are closed.

« »